Lipid Care Tea
Viungo:
Herba Gynostemmae Pentaphylli, Folium Nelumbinis, Radix Polygoni Multiflori, Green Tea, Semen Cassiae, Radix Rehmanniae Preparata
Kazi Na Faida Zake
- Kurekebisha kiwango cha lipids katika damu;
- Kusaidia kuvunjavunja na kujenga lipids na kubadilisha lipid kuwa nishati, na kusaidia kupunguza unene;
- Kuondoa sumu na kuurembesha mwili
Yafaa Kutumika Kwa:
- Watu wenye historia ya kuwa na lipids katika koo zao
- Watu wenye unene au uzito wa kupitiliza
- Watu wenye mafuta kwenye ini
Maelezo Muhimu:
Kuwa Na Lipid Ya kuzidi Katika damu - Hyperlipidemia:
Utafiti wa karibuni umeonyesha kuwa uzidifu wa lipid katika damu ndicho chanzo kikuu cha magonjwa ya moyo, ini kuwa na mafuta (fatty liver) na unene, na magonjwa ya moyo kuongoza katika kuhatarisha maisha ya binadamu. Lipid ni namna ya mafuta ambayo ni kiungo muhimu katika ujenzi wa seli za mwili. Kulingana na takwimu, asilimia 30 ya watu wenye umri zaidi ya miaka 15 wana tatizo la kuwa na pressure ya juu, watu wenye umri wa zaidi ya miaka 18 wana matatizo ya ukubwa tofauti ya kuziba kwa mishipa ya damu, mtu mmoja hupoteza uwezo wa kutembea kila baada ya sekunde 4 na mtu mmoja hufa kutokana na ugonjwa huo kila sekunde 16. Sababu kubwa ni kuwa na lipid kupita kiwango kunakosababisha matatizo ya mzunguko wa damu.
Mafuta ndani ya damu zetu huitwa lipids. Lipids huungana na protini ndani ya damu na kutengeneza lipoproteins. Lipoproteins ni chanzo cha nishati kwa miili yetu kwa hiyo ni muhimu kwetu.
Kuna aina tatu ya liproproteins ndani ya damu zetu. High-density cholesterol (HDL), low-density cholesterol (LDL) na very low-density cholesterol (VLDL). HDL huitwa ni cholesterol nzuri kwa sababu huzuia cholesterol kujijenga kwenye mishipa yetu ya damu. LDL ni cholesterol mbaya kwa sababu kiwango kikubwa cha LDL katika damu kinaongeza uwezekano wa kupata kiharusi au magonjwa ya moyo. Tunasema una lipids kwa wingi pale unapokuwa na viwango vikubwa vya LDL na mafuta yaitwayo triglycerides . Watu wenye LDL cholesterol na triglycerides kwa wingi wanakuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa ya mishipa ya moyo na magonjwa ya mishipa ya ubongo.
Uzidifu wa lipid katika damu na unato wa damu husabisha kutokea kwa chembechmbe katika damu; kunywea kwa mishipa ya damu husababisha kuziba kwa mishipa; kuta za mishipa huwa nyembamba na ngumu na hukosa mnyumbuko. Cholesterol na triglycerides vikizidi katika damu husababisha cholesterol kutuama juu ya kuta za mishipa ya damu na kutengeneza utando kwenye arteri, kuziba mishipa ya damu, matatizo ya mzunguko wa damu na kusababisha magonjwa mbalimbali.
Makundi ya watu yaliyo kwenye hatari ya kuwa na lipids kwa wingi ndani ya damu zao ni; watu wanaokula sana, watu wanaovuta sigara kwa muda mrefu, watu wanaotumia pombe kwa muda mrefu, watu wanaofanya kazi za kukaa kwa muda mrefu, watu wenye umri mkubwa na watu wenye msongo wa mawazo.
Hyperlipidemia Kusababisha Cirrhosis
Kuwepo kwa lipids nyingi kuliko kiwango (hyperlipidemia) kunaweza kuleta madhara kwenye ini na hali hiyo ikienda kwa muda mrefu husababusha matatizo ya kuwa na mafuta kwenye ini (fatty liver), na baadaye kutuama kwa mafuta juu ya mishipa ya ini hudhuru ini na ini likishadhurika umbo lake hubadilika na kuwa na makovu (cirrhosis) na kuleta madhara kwenye ufanyaji kazi wake.
Hyperlipidemia Kusababisha Unene
Hyperlipidemia inaweza kusababisha kunenepa kupita kiasi. Lipids katika mwili zikizidi kiwango cha kawaida, kiasi kukubwa cha lipids kitakuwepo ndani ya damu chini ya ngozi na kuzunguka eneo la ndani ya mishipa ya damu, na kusababisha mafuta kutolewa kwa wingi, na hivyo kusababisha mwili kunenepa.
Herba Gynostemmae Pentaphylli: Mmea huu unaboresha uvunjwaji na ujenzi wa kemikali katika mwili, huimarisah kinga za mwili na una nguvu ya kimaajabu ya kutunza afya ya mwili, kupunguza lipids mwilini, kurekesha pressure ya mwili, kupunguza uzito wa mwili, kuzuia kuganda kwa mafuta kwenye mishipa ya damu na magonjwa ya moyo. Una tabia ya antioxidant, ya kuondoa uchovu, kuondoa madhara ya dawa za homoni, kuongeza hamu ya kula , kuboresha usingizi, kurutubisha nywele na ngozi, kuzuia kuzeeka haraka, n.k.
Semen Cassiae: Mmea huu una tabia ya kuongeza uwezo wa kuona, kupunguza lipids, kusaidia utoaji wa uchafu mwilini, na kupunguza unene. Utafiti umeonyesha kuwa mmea huu unapunguza pressure ya mwili na lipids katika damu, unaua bakteria, una unaweza kutumka katika kuondoa tatizo la hyperlipidemia.
Radix Polygoni Multifori: Utafiti wa karibuni umeonyesha kuwa radix polygoni multiflori ni mmea unaoweza kupunguza kasi ya kuzeeka, kurekebisha lipids katika damu, kuzuia kuganda kwa mafuta katika mishipa ya damu, na kuongeza kinga za mwili, n.k. Katika kurekebisha kiwango cha lipids mwilini, unapunguza uwingi wa low density lipoprotein ambayo ina madhara katika mwili, unaongeza kiwango cha high density lipoprotein ambayo ina manufaa kwa mwili. Unapunguza pia ufyonzwaji wa cholesterol na utumbo, na kupunguza madhara ya atherosclerosis.
Folium Nelumbinis (Lotus Leaf): Mmea huu unasaidia kuondoa lipids. Una tabia ya kusaidia kuondoa mabaki ya chakula (kinyesi) na mkojo kutoka ndani ya mwili, unasaidia kuondoa sumu kutoka kwenye utumbo, unapunguza lipids, unaondoa grisi, na kupunguza glycerin na cholesterol kwenye majimaji ya mwili.
Radix Rehmanniae Preparata: Moja ya dalili ya matatizo katika ufanyaji kazi wa ini na figo ni kuwashwa na kukosa nguvu kiunoni na kwenye magoti, homa, kutoa jasho usiku na kutokwa na manii. Tiba asili ya China (TCM) inaamini kuwa kuna baadhi ya magonjwa yanahusishwa na udhaifu wa figo, kama kisukari, kutokwa damu kwenye uterus, upungufu wa chembechembe nyekundu za damu, mapigo ya moyo kwenda mbio, matatizo ya hedhi, kizunguzungu, mlio kwenye masikio na kuota mvi mapema. Radix rehmanniae preparata hurutubisha figo na ini kwa kupeleka damu na vitu muhimu.
<<<<< MWANZO